KIMUHEMUHE kilitanda kwenye viunga vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana Feb 17, 2017, kufuatia ndugu, jamaa na marafiki wa model, Agness
Masogange kufurika huku wakitarajia kumuona ndugu yao huyo akifikishwa
mahakamani hapo.
Ndugu hao waliwasili Kisutu mapema asubuhi na kuweka kambi mahakami ili
kusikiliza kesi ya masogange anayehusishwa na... tuhuma za matumizi ya dawa
za kuleya.
Licha ya Masogange kutokufikishwa mahakamani hapo kwa kile kinachodaiwa
kuwa majibu ya Mkemia Mkuu wa Serikali kuhusu kipimo endapo mwanadada
huyo anatumia madawa ya kulevya, kilikuwa hakijatoka lakini mpaka
ilipotimu majira ya saa 9:00 mchana, ndugu hao walikuwa hawajakata
tamaa. Baada ya kuona hakuna dalili zozote kwa ndugu yao kuletwa
mahakamani hapo huku muda wa mahakama wa saa 9:30 ukiisha, ndipo ndugu
hao waliamua kuondoka kwa unyonge eneo la Kisutu.
Taarifa iliyotolewa jana na Kamnada wa Polisi Kanda Maalum ya Dar,
Kamishna Somon Sirro ilieleza kuwa, Masogange na wenzake 17,
wanashikiliwa na jeshi hilo kwa tuhuma za kuhusika na matumizi ya dawa
za kulevya, na kwamba jana walipelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serkali kwa
ajili ya vipimo na endapo ikibainika wanatumia madawa ya kulevya, leo
Ijumaa au Jumatatu ijayo watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma
zinazowakabili.
0 comments:
Post a Comment