Nyota wa Tanzania na klabu ya KRC Genk ya Ubeligji, Mbwana Samatta
ameongeza hatua katika rekodi ya idadi ya mechi ndani ya klabu yake hiyo
baada ya jaan usiku kucheza mechi yake ya 80 katika mashindano yote,
tangu ajiunge na timu hiyo.
Samatta ambaye alijiunga na KRC Genk Januari 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ametimiza mechi hizo wakati timu yake ikipokea kichapo cha bao 1-0 kutoka...
kwa Club Bruge kwenye mchezo wa ligi kuu ya Ubeligji.
Katika mchezo wa jana kwa mara ya kwanza Samatta amechezeshwa dakika zote 90 za mchezo tangu apone maumivu ya goti aliyoyapata Novemba mwaka jana. Katika mechi hizo 80, Samatta ameifungia Genk mabao 20 katika mashindo yote.
Matokeo hayo ya 1-0 yameiacha Genk katika nafasi ya 6 kwenye kundi A, la ligi ya Ubeligji ambayo ipo katika hatua ya mtoano ya kumsaka bingwa pamoja na timu za kuwakilisha nchi kwenye mashindano ya kimataifa. Club Bruge ndio vinara wa kundi hilo.

0 comments:
Post a Comment