Klabu ya Real Madrid hapo jana usiku ilifanikiwa kuchomoza na ushindi mujarabu wa mabao 3 – 0 dhidi ya Juventus mchezo wa klabu bingwa Ulaya uliopigwa nchini Italia.
Licha ya ushindi huo mnono bao la pili lililofungwa na mshambuliaji wa timu hiyo, Cristiano Ronaldo limezua gumzo kubwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii huku kocha wa timu hiyo, Zinedine Zidane akisema kuwa mchezaji huyo bora wa duniani na mshindi mara tano wa tuzo za Ballon d’Or ni miongoni mwa...
wachezaji bora na wenye historia kubwa kwenye mchezo wa soka.
Unaweza kusema kuwa yeye ni mmoja wa miongoni mwa wachezaji bora kuwahi kutokea katika historia ya soka duniani. Muda wote huwonyesha kuwa yeye ni mhcezaji wa kipekee na mara zote hupenda kufanya vitu bora katika michuano ya Champions League na hajawahi kuchoka kufanya hivyo.
Cristiano yupo kwenye kiwango bora kwa sasa na hata wachezaji wenzake wanafurahishwa na uwezo wake. Tunahitaji kufurahi usiku huu na kufikiria kazi kubwa na ngumu mbele yetu wiki ijayo kwa kuwa Juve hawajakata tamaa.
Meneja wa Juventus, Massimiliano Allegri kwa upande wake amesema kuwa, Hana hakika kama bao la Ronaldo ni bora zaidi kwenye historia ya soka.
Sina hakika kama goli la Cristiano ni bora zaidi kwenye historia ya soka lakini ni lakizazi kingine kabisa. Anapaswa kupewa pongezi kwakile alichokifanya.
Nimesikitishwa na bao la tatu namna lilivyopatikana kwakuwa naamini kama yangebaki mawili lazima tungepambana na kurudisha lakini kwa sasa haitowezekana.
Ronaldo anakuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao 10 kwenye mchezo wa Champions League.
Bao la tatu limefungwa na Marcelo dakika ya 72 , mchezo wa marudiano unatarajiwa kufanyika huko Bernabeu siku ya Jumatano ya Aprili 11 wakati mlindalango wa Juventus, Gianluigi Buffon akitarajia kuwa uwanjani kwa mara ya mwisho na kutundika daluga kwenye soka.
0 comments:
Post a Comment