NI fununu tu! Mwanamuziki wa kizazi kipya, Juma Jux, ameweka bayana kile
kinachoendelea kati yake na Vanessa Mdee ‘V Money’ kuwa ni mambo ya kikazi
na si uhusiano wa kimapenzi.
Akizungumza katika mahojiano maalum na Global TV Online, Jux aliyasema
hayo kutokana na tetesi zilizokuwa zikiandikwa kwenye mitandao ya
kijamii, kwamba amejiweka kwa mwanadada huyo anayetamba na... Wimbo wa Siri
alioshirikiana na Barnaba.
“Ni fununu tu, hakuna jingine. Mimi na Vanessa tupo kikazi, nakumbuka
nilipokuwa nataka kufanya video yangu ya Sisikii, nilikuwa natafuta
msichana wa kuwa naye kwenye video, kwa sababu alikuwepo, basi hakukuwa
na jinsi, nikaamua kumtumia kwani aliujua wimbo vizuri hivyo nikaamini
kwamba video ingekuwa poa sana na kweli ikawa hivyo,” alisema Jux.
0 comments:
Post a Comment