Pages

Subscribe:

Monday, November 28, 2016

MWANA FA: DUME SURUALI ILIKUWA INAITWA SITOI HELA


15099330_914188058682108_8839950530995290112_n
Hapo mwanzo, wimbo wa Mwana FA, Dume Suruali ulikuwa ukiitwa Sitoi Hela. Akiongea kwenye kipindi cha Ngaz Kwa Ngaz cha EATV wiki iliyopita, Mwana FA alidai kuwa Sitoi Hela ulikuwa na maneno makali kiasi ambacho kutokana na kuhofia kuwakera wanawake wengine alilazimika kubadilisha mistari mingi.

“Kuna kitu kilitokea huko nyuma mtaani, kuna neno ‘unajua bana sisi staff’ Sisi staff kwa maana ya kwamba unajua staff wale wanapanda kwenye daladala kwamba ‘mimi staff wa gari gani’ sasa wanakuwa hawalipi. So nikafiria...
kwamba staff kwa maana kwamba hatutoi hela,” alisema FA.

“Kwahiyo idea ya kwanza wimbo ulikuwa unaitwa ‘Sitoi Hela’ na niliurekodi kabisa na wimbo ukawa umekamilika. Baadaye tukaja kufikiria ‘kwamba hii ngoma kali lakini it’s too harsh. Hii wasichana huko barabarani wanaweza wakatembea na majivu na masizi wanikamate wanisute na chupa za maji, wanipige. Kwahiyo how do we do it? Tutengeneze balance, beside si tu wanaume suruali, kuna watu wanakuwa si tu hawataki kuhonga, wanataka kuhongwa wao,” aliongeza.

Dume Suruali aliyomshirikisha Vanessa Mdee inafanya vizuri kwa sasa kwenye redio na TV na tayari ina zaidi ya views lakini mbili tangu iwekwe mwishoni mwa wiki.

0 comments:

Post a Comment