Wiki
iliyopita, Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group,
Ruge Mutahaba, alidai kuwa vituo vyake vinaweza kuanza kucheza kazi za
Lady Jaydee iwapo akiwaruhusu wafanye hivyo.
Kupitia Instagram, Lady Jaydee ameijibu ofa hiyo kwa dongo
lililowaendea wasanii waliowahi kumshirikisha kwenye nyimbo zao lakini
kwa kuogopa kuingia matatani na...
kituo hicho chenye nguvu nchini,
walifuta sauti yake.
“Kwahiyo wale mlio omba collabo sijui feat baadae mkaenda kufuta
chorus zangu mtafanyaje ? Habariiiiiiiiiii zenu buaaaaaana #SawaNaWao
#TofautiNaHesabuZao,” aliandika Jide.
Ruge alitoa kauli hiyo Ijumaa iliyopita kwenye mahojiano na kipindi cha XXL.
“Tatizo ni kwamba hakuna ambacho hatujamaliza, tulimaliza, tunasubiri
order. Unajua kimsingi ulipopewa order ya kwamba ‘nyimbo zangu usipige,
jina langu usiseme kwenye chombo chako, vyovyote itakavyokuwa mimi
sitaki kusikia hiyo kitu’ hiyo ndio order. Kwahiyo labda tukikutana,
nimuombe tena [Lady Jaydee] kama tutaruhusiwa kufanya hiyo kitu,”
alisema.
Ruge pia alisema ana muda mrefu hajawahi kukutana na Lady Jaydee,
japo amedai ‘hata leo nikipata nafasi ya kahawa nitashukuru sana kwa huo
mwaliko.’
Wiki kadhaa zilizopita Ruge na Joseph Kusaga walishinda kesi ya
kuchafuliwa (defamation) iliyokuwa imefunguliwa dhidi ya Lady Jaydee na
muimbaji huyo kuamriwa kuwaomba radhi.
“Tunashukuru walau tulishinda ile kesi lakini at least ilitengeneza
mfano wa watu kuelewa kwamba tusipende kutuhumu vitu kama watu huna
uhakika. Bahati nzuri pia hata katika hiyo kesi alisema mwenyewe
hajawahi kusikia tunasema, aliambiwa na watu. Lakini ni mambo yashapita
hayo.”
Monday, November 28, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment