Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) ambalo husimamia wasanii pamoja na
kazi zao ikiwa ni wasanii wa filamu pamoja na wale wa muziki limesema
kuwa linapitia video mpya ya mwanamuziki Rich Movoko aliyomshirikisha
Diamond Platnumz kuona kama kuna vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia.
BASATA kupitia ukurasa wao wa Twitter wameandika kuwa wapo thabiti
kusimamia maadili katika sanaa na udhalilishaji wa wanawake. Aidha
wameeleza kuwa video hiyo iliyotoka jana usiku inayokwenda kwa jina la
Kokoro ipo katika... uhakiki kujionea kama picha za wanawake waliomo kwenye
video hiyo zinakiuka maadili ya kitanzania na muda si mrefu watatoa
taarifa.
BASATA wamekuwa wakiwafungia wasanii wengi wanaokiuka maadili ya sanaa
ambapo miongoni mwa wasanii wengi waliofungiwa ni pamoja na Nay wa
Mitego, Snura huku wengine wakipewa onyo na video nyingine kuzuiwa
kuchezwa mchana kwa mfano Zigo Remix ya AY Ft. Diamond Platnumz na
Asanteni Kwa Kuja ya Mwana FA.
Wednesday, November 23, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment