MAREKANI: Rapper maarufu nchini
Marekani aliyewahi kutangaza nia ya kugombea urais wa nchi hiyo mwaka
2020, Kanye West, jana Jumatatu Novemba 21 alilazwa katika hospitali
moja iliyoko jijini Los Angeles baada ya kuugua ghafla.
Tatizo hilo limetokea ikiwa ni siku
chache baada ya kukatisha show zilizokuwa zimesalia za ziara yake ya
Saint Pablo kutokana na kukabiliwa na...
uchovu.
Vyanzo vya taarifa hiyo kikiwemo, TMZ na FoxNews.com,
na NBC News, Kanye alipelekwa hospitalini baada ya polisi kupigiwa simu
nyingi za dharura na watu mbalimbali wakieleza haliya staa huyo, ndipo
wakafika kumchukua na kumpeleka hospitali.
West amegonga headlines kwa
kauli tata alizozitoa wakati wa show zake mbili zilizopita ikiwemo
kuwatukana Jay Z na Beyonce, Hillary Clinton, Mark Zuckerberg, radio na
MTV huku akimfagilia Donald Trump wakati akimalizia shoo iliyopewa jina
la Sacramento na kusema maneno haya “would have voted for Donald Trump”.
Msemaji wa West ameeleza jana kuwa,
wamesitisha shoo zote zilizokuwa zimesalia licha ya kutotaja sababu ya
kufanya hivyo. West atapata hasara ya zaidi ya dola milioni 10 kutokana
na kukatisha shoo hizo.
Familia yake ipo kwenye wakati mgumu kwa
sasa. Mwezi uliopita, mkewe Kim Kardashian, alivamiwa kwa mtutu wa
bunduki na kuporwa mali huko Paris, Ufaransa.
0 comments:
Post a Comment