Meya wa Jiji la Mbeya, Mchungaji David Mwashilindi ambaye ni kiongozi wa Kanisa la International Evangerism Assemblies of God, amesema migogoro ndani ya... madhehebu, uroho wa madaraka na utapeli ni miongoni mwa sababu ya watu kuamua kuanzisha madhehebu kila kukicha.
Meya huyo ambaye pia ni msimamizi wa kanisa hilo katika mikoa ya Ruvuma, Iringa, Njombe na Rukwa, amesema hakuna ubaya wa kuwa na madhebu mengi kama yanaanzishwa kwa kufuata utaratibu, sheria na misingi ya Mungu.
Amesema madhehebu mengi ya kilokole jijini humo yaliibuka baada waamini kuamua kujitenga madhehebu yao ya awali kutokana na migogoro.
“Kuna madhehebu yanamiliki vyuo vya wachungaji wanaosomea kwa mujibu wa maadili ya Mungu, kama Lutherani, Wakatoliki, Moravian, Wasabato na la kwangu, lakini tatizo wapo wachungaji wa kujipachika ambao mara nyingi wanatiliwa shaka kwa vitendo vyao,” amesema meya huyo.
0 comments:
Post a Comment