Pages

Subscribe:

Monday, March 5, 2018

KWA MARA YA KWANZA SASA WANAWAKE NCHINI SAUDI ARABIA WARUHUSIWA KUKIMBIA

Baada ya Wanawake kuruhusiwa kuingia uwanjani kushabikia mpira wa miguu kwa mara ya kwanza tena Leo March 5, 2018  nakusogezea stori kuhusu Wanawake nchini Saudi Arabia kwa mara ya kwanza katika historia wameshiriki mashindano ya kukimbia.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo, mashindano hayo yalikuwa ya Kilomita 3 yamefanyika mashariki mwa...
Al Ahsa.

“Al-Ahsa Runs” lilikuwa ni jina la marathon ambayo ilihusisha wanawake 1,500 katika makundi mbalimbali kama vile kitaaluma, amateur, wazee na vijana.

Katika mashindano hayo Mizna al-Nassar wa Saudi Arabia alishinda medali ya kwanza katika marathon, akiwaacha nyuma wapinzani wake kutoka katika mataifa tofauti.

0 comments:

Post a Comment