Rapper kutoka nchini Marekani anayeunda kundi la Ruff
Ryders, DMX amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kosa la kukwepa
kulipa kodi.
DMX alikamatwa July mwaka jana, kwa mujibu wa CBS rapper
huyo anadaiwa kiasi cha dola milioni 1.7 ambapo inasemekana alifungua
akauti benki nyingine na kutumia jina jingine ili kukwepa...
kodi.
DXM alikuwa akikabiliwa na mashtaka 14 ya ukwepaji kodi,
hata hivyo alilipa faini ya dola 5000,000 za Kimarekani kinyume na hapo
angetumikia kifungo cha miaka 44 jela.
Imeripotiwa
kuwa DMX ameingiza zaidi ya dola milioni 2.3 kwa mwaka 2010 hadi 2015
lakini msanii huyo alikwepa kulipa kodi. Rapper huyo ni baba wa watoto
15.
0 comments:
Post a Comment