Muigizaji wa filamu mwenye nyota yake bongo na Afrika Mashariki Wema
Sepetu, amedai amevumilia matusi vya kutosha anayotukanwa na kupitia
mitandao ya kijamii bila kosa lolote hivyo kwa sasa ataenda nao hatua
kwa hatua.
Wema Sepetu ametoa kauli hiyo alasiri ya jana (Machi 16, 2018) baada ya baadhi ya watu kupenda kumtolea maneno machafu na kumdhihaki kwa jambo ambalo yeye...
hakupenda awe nalo au limfike katika maisha yake.
"Naona mmeshanikariri hua nakaa kimya pale mnapo ona 'comment' ya matusi, nimepuuzia kwa muda mrefu mno ila tukumbuke kuwa na mimi nina moyo ambao una nyama tena ni binadam kama nyie tu. Kama vile usivyopenda kuona mtu anakukebehi basi ndio hivyo hivyo ninavyo 'feel', kwani lazima matusi?, hakuna asiyejua kutukana kwenye ulimwengu huu tena midomo michafu haswa ila tunajitahidi kujistiri", amesema Wema.
Aidha, Wema Sepetu amesema hakuna jambo ambalo linamkera kupita kiasi kama kuona anatukanwa kupitia 'social media' tena kwenye ukurasa wake mwenyewe.
"Kwani kuna ulazima ku-coment tena matusi 'sometimes' mtu anaweza 'ku-push ur buttons to the extent when it comes to me nina extents' zangu 'and u don't go there', navumilia vingi mno jamani kweli kweli. 'Try putting yourselves in my shoes for a minute and see if they fit'. Ukipost kitu chako kuna ile mijitu iliotapikwa inakuja na maneno yao ya chooni utasema imetumwa. Kwani ni mashindano?, sio poa jamani", amesisitiza Wema.
Kwa upande mwingine, Wema Sepetu amewakumbusha baadhi ya watu wenye tabia hiyo kuwa naye ni binadamu kama walivyo wao na mwenye moyo wa nyama na wala sio chuma hivyo anasikia maumivu makali kama wayapatao wao pindi wakitukanwa katika mitandao ya kijamii.

0 comments:
Post a Comment