skip to main |
skip to sidebar
WATANZANIA WALIONYIMWA VIZA ZA KWENDA UK WALIPWA FIDIA
Uongozi wa kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa
leo imetangaza kuwalipa fidia ya Tsh milioni moja kwa kila mtanzania
aliyekuwa kashinda zawadi ya kwenda kutazama game za Ligi Kuu England LIVE wakiwa uwanjani.
Kampuni hiyo imeshindwa kutimiza ahadi yake kwa washindi wake kuwapeleka England kutazama mechi za EPL kwa timu wanazozidhamini kama Southampton, Arsenal, Everton na Hully City kutokana na ubalozi wa England kutokubali...
kutoa visa kwa washindi hao licha ya jitihada hizo kufanyika.
Mkurugenzi wa utawala na utekelezaji Abbas Tarimba
amethibitsha hayo na kueleza kuwa kampuni hiyo, kwa mujibu wa kanuni
zao wameamua kutoa kifuta jasho cha Tsh milioni 1 kwa kila mshindi kama
kanuni zao zinavyowaagiza.
0 comments:
Post a Comment