Uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 70,000, kwa zaidi ya miaka 10 umekua ukitumiwa na jeshi la kulinda amani nchini Somalia hali ambayo inazuia... shughuli za kimichezo kuendelea uwanjani hapo.
Raisi wa chama cha soka nchini Somalia Abdiqani Said Arab, ameliambia shirika la utangazaji la Uingereza BBC, tayari wameshafanya mazungumzo na wakuu wa jeshi la kulinda amani nchini humo tangu mwaka 2013 na sasa wamerejea tena kufanya hivyo.
Said Arab amesema umefika wakati kwa majeshi hayo kutafuta mahala pengine pa kuweka kambi nasi uwanjani hapo, kutokana nan chi ya Somalia kuhitaji kujiendelea kimichezo, hasa kwa vijana ambao wamekua na kitu ya kushirikishwa kikamilifu katika sekta hiyo.
Kiongozi huyo ameendelea kutanabaisha kwamba, kwa muda wa miaka mingin, Somalia imekua inashindwa kushiriki katika michuano ya awali ya fainali za mataifa ya Afrika, kutokana na kukosa sifa ya kuwa na uwanja wa nyumbani.
Wakati SFA kupitia kwa raisi wao wakisisitiza jambo hilo, uwanja wa taifa wa Somalia una viwanja vya michezo mingine kama mpira wa kikapu(basketball), mpira wa wavu (Volleyball) pamoja na mabwawa ya kuogelea.
Kwa mara ya mwisho uwanja huo uliacha kutumika kama sehemu ya michezo nchini Somalia mwanzoni mwa miaka ya 1990, baada ya jeshi la Marekani kuweka ngome katika uwanja huo ambao pia ulitumika katika filamu inayoonyesha vita kati ya majeshi hayo dhidi ya wasomali iitwayo Black Hawk Down.
0 comments:
Post a Comment