Mastaa warembo kutoka Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu na
Jacqueline Wolper Massawe, wamejikuta wakipiga ulabu hadi kulewa
chakari, kisa kikielezwa kwamba wana msongo wa mawazo.
Tukio hilo lilijiri hivi
karibuni, usiku mnene kwenye pati ya kuzaliwa (birthday) ya meneja wa
kampuni ya Wema ya Endless Fame almaarufu Petit Man iliyofanyika kwenye
nyumba ya...
jamaa mmoja maeneo ya Kinondoni-Manyanya jijini Dar na
kuhudhuriwa na mastaa kibao.
Katika pati hiyo ambayo mbali na mastaa ilihudhuriwa na watoto wa mjini,
watu waligonga msosi wa kufa mtu kisha vikafuata vinywaji.
Tofauti na ‘maraia’ wengine, Wema na Wolper walikuwa wakigonga
vinywaji vikali hadi wakawa tilalila na kuanza kufanya vituko, jambo
ambalo liliwashangaza wengi.Kadiri muda ulivyokuwa unasonga ndivyo
mastaa hao walivyozidi kucharuka tofauti na walipofika kwani walionekana
wapole na wastaarabu kupita maelezo.
Baada ya ulabu kuwakolea walianza kupigana picha kwa simu kisha
kukata mauno kabla ya Wolper kuzimika kufuatia kuzidiwa na
‘kinywaji’.Kwa upande wake Wema alimpiga vibao mwanaume shoga aliyetajwa
kwa jina moja la Danny baada ya kutibuana kabla ya watu
kuwaamulia.Ulipofika muda wa kuondoka mahali hapo, ilidaiwa kwamba
Wolper ilibidi abebwe ili kupelekwa kwenye gari kwani alikuwa hajiwezi.
Uchunguzi wa gazeti hilo umebaini kwamba, mastaa hao wana msongo wa
mawazo hivyo wanaona njia pekee ya kuwaondolea ‘stresi’ ni kunywa pombe.
Habari za ndani zilieleza kwamba, tangu Wema ameachana na staa wa
Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amekuwa mtu mwenye mawazo
na njia pekee ambayo huitumia ni kujipooza kwa pombe kali.
“Ndiyo maana ana mpaka kaunta ya pombe kali nyumbani kwake,” alisema mmoja wa watu wake wa karibu (Team Wema).
Ilisemekana kwamba mbali na mawazo ya Diamond ambaye amehamia kwenye
nyumba ambayo Wema alikuwa na mchango mkubwa wakati wa ujenzi, pia suala
la jamaa huyo kutanua na mpenzi wake wa sasa, Zarinah Hassan ‘The Boss
Lady’ limekuwa likimpa wakati mgumu mwanadada huyo.
Habari zilieleza kuwa, jambo lingine linalompa Wema msongo wa mawazo
ni suala la kukosa mtoto kila anapomtafuta akiamini kuwa watu wanajua
yeye ni mgumba.Pia ilielezwa kwamba kuna suala la kuishiwa na kuogopa
kufilisika kwani kwa sasa filamu hazilipi na bado anataka kuendelea kuwa
na heshima ya kuitwa Madam hivyo njia pekee anayoona inafaa kutuliza
mawazo ni kunywa pombe.
Kwa upande wake Wolper uchunguzi ulionesha kwamba, kwanza anapenda
fedha hivyo kukosa tenda za kuigiza na kuanguka kwa soko la filamu za
Kibongo kumemsababishia msongo wa mawazo kama ilivyo kwa Wema kwani naye
anataka kuishi maisha ya kistaa ambayo hayawezekani bila kuwa na
mshiko.
Akizungumzia hali hiyo, Wolper alikiri kuwa na mawazo mengi huku akihisi kuwa huenda amelogwa
Sunday, April 19, 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment