Staa wa Bongo Movies, Moshi Katemi ‘Mo Music’, amesema
anatamani kumshirikisha staa mrembo wa Bongo Movies, Elizabeth Michael
‘Lulu’ katika muziki wake kwa kuwa anampenda. Msanii huyo aliyewahi kutamba na wimbo wa ‘Basi Nenda’, alisema
ametokea kumpenda mrembo huyo kutokana na...
umahiri wa kazi zake za
filamu, maana uwezo wake una tofauti kubwa na waigizaji wengine.
Mo Music aliongeza kwamba huwa ana kawaida ya kutazama filamu za wasanii
mbalimbali, lakini za Lulu humvutia zaidi kiasi kwamba anatamani
ashiriki kama ‘video queen’ katika muziki wake.
“Ninafuatilia kazi za wasanii mbalimbali, ila kwa Lulu ni tofauti,
natamani nimshirikishe katika video za wimbo wangu mpya wa ‘Nitazoea’
kwa kuwa naamini ana mvuto mkubwa,” alimaliza Mo Music
Wednesday, April 15, 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment