Muigizaji wa filamu, Elizabeth ‘Lulu’ Michael mwenye wafuasi wengi
kwenye Instagram, ameamua kujiondoa baada ya kushambuliwa kwa matusi na
baadhi ya watu kufuatia kifo cha mtu aliyewahi kuwa mpenzi wake.
Kufuatia kifo cha kutatanisha cha Lusekelo Samson Mwandenga ‘Secky’,
watu wengi walianza kumtukana Lulu wakimhusisha pia na kifo hicho huku
pia wakipost picha zinazomuonesha alipokuwa na marehemu...
Hata hivyo mujibu wa Global Publishers, familia ya Secky imeweka wazi chanzo halisi cha kifo chake.
Familia hiyo imeeleza kuwa marehemu aliumizwa na kiti cha kioo akiwa
kambeba mtoto wake nyumbani kwake kisha akapelekwa hospitali na baadaye
kufariki dunia akiwa huko.
Katika hatua nyingine msanii mkongwe wa filamu, William Mtitu amefunguka
na kuwataka watu kuacha kumshambulia Lulu kwa kitu ambacho hahusiki
nacho.
“Lulu ni msanii mdogo sana kiumri na amepitia mitihani mikubwa sana
katika maisha ambayo mimi na wewe kabda tusingeiweza kuikabili plz
nawaomba tumuache kwa sasa inatosha jamani kumbukeni huyu ni binadamu na
moyo kama nilivyokuwa mimi na wewe hivi utajisikiaje km utasikia lulu
amejizulu kwa namna yeyote ile kutokana na maneno yako ya kumshambulia
mitandaoni,” ameandika kwenye Instagram.
“Kumbukeni sisi ni banadamu atuijui leo yetu itaishaje wala kesho yetu
itakuwaje? Plz inatosha sasa watanzania wenzangu. MTAARIFU NA MWINGINE.”
Miaka miwili iliyopita Lulu aliwahi kukaa jela kutokana na kushtakiwa
kwa kumuua bila kukusudia Steven Kanumba aliyekuwa mpenzi wake.
Saturday, April 18, 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment