Mwigizaji katika tasnia ya filamu Tanzania Irene Uwoya amesema kuwa
filamu zimeharibu mipango yake ya miaka mingi ya kutaka kuwa mwongozaji
wa ndege yaani Rubani.
Irene alisema hayo weekend hii kupitia kituo cha Radio cha East Africa
Radio na kudai kuwa miaka yote aliyokuwa akisoma lengo lake kubwa
lilikuwa ni kuja kuwa muongozaji wa ndege Rubani kwani ndiyo kazi
aliyokuwa akiipenda na alianza kusoma masomo ambayo aliamini moja kwa
moja... yangeweza kumfanya kufikia ndoto hizo.
Amesema ndoto yake hiyo iliingia ukakasi baada ya kuanza kufanya filamu
za bongo na kujikuta sasa maisha yake yapo kwenye filamu zaidi.
Irene uwoya ambaye alikuwa ni mke wa ndoa wa mchezaji mpira Sulemani
Yamin Ndikumana alisema kati ya mwaka 2007 na 2008 ndipo alipoingia
katika tasnia ya filamu ambapo anadai kuwa hakuichukulia serious kazi
hiyo, sababu tayari alikuwa na mipango ya kusoma na kuja kuwa rubani
lakini aliamua kuingia katika tasnia hiyo kufuatia kushawishiwa na
baadhi ya watu ambao waliamini kuwa anaweza kuigiza.
"Katikati ya mwaka 2007 na 2008 ndipo niliingia katika tasnia ya filamu
nchini tena kwa kushawishiwa na baadhi ya watu, ila mimi nilikuwa
nafanya tu sikuwa serious kabisa maana mimi malengo yangu yalikuwa
nisome nije kuwa rubani, lakini baada ya kuanza kufanya nikaona watu
wananikubali na kupenda kile nikifanyacho na nilipoanza kupata mafanikio
nikaona okay kumbe hii ni kazi nikaanza kufanya kazi sasa."
"Nikajikuta sasa maisha yangu yote yameegemea katika filamu na nikaanza
kufanya filamu kama maisha mpaka sasa, ingawa kuna kipindi nilikuwa
kimya kidogo kutokana na matatizo ya ndoa yangu, maana hakuna kitu
kilikuwa kinanitesa kama maneno ya watu, ilifika kipindi nilikuwa siwezi
kufanya jambo lolote kwa kuhofia watu, maana nilikuwa naona kama watu
wananizungumzia mimi, hivyo kipindi kile kilinirudisha nyuma kidogo,
lakini nashukuru Mungu baadaye niliona ni suala la kawaida, maana kuna
watu wengi walikuwa katika ndoa na mwisho wa siku ndoa zao zilivunjika
na maisha yaliendelea kuanzia hapo ndipo nilipata nguvu na kurudi
kuendelea na kazi kama awali, ila kipindi hicho kwa kweli kimenipa taabu
sana" Aliongeza Irene Uwoya.
Mbali na hapo Irene alizidi kuweka wazi kuwa kupitia filamu amefanya
mambo ya maendeleo mengi sana ikiwepo kuishi maisha yake ayatakayo yeye
pasipo kumtegemea mtu yoyote, lakini pia filamu zimeweza kumjengea
nyumba ambayo anadai nyumba hiyo inakamilika muda si mrefu tokea sasa.
Amesema hiyo ni mbali na ziara nyingi na mialiko mingi aipatayo nje ya
nchi ambayo nayo humjenga na kumpa nafasi zaidi katika kukutana na watu
ambao nao wanakuwa na msaada katika kumtengenezea network nzuri ya kazi
yake ya sanaa.
Licha ya kuzungumzia mambo mazuri ambayo ndani ya tasnia ya bongo movie
lakini Uwoya alisema kuwa kwa sasa tasnia hiyo inaingiliwa na watu ambao
wengi wao hawana vipaji wala uwezo wa kuigiza na wanapewa nafasi jambo
ambalo linasababisha tasnia hiyo kushuka chini, hivyo anadai kuwa kwa
sasa ana mpango wa kukaa na wasanii wenzake.
wakubwa ili waweke mpango wa kuona jinsi gani wanaweza kuzuia watu wasio
na vipaji kutoingia katika tasnia hiyo na kuiharibia jina tasnia ya
bongo movie ambayo imeweza kubadili maisha ya vijana wengi na kutoa
ajira pia kwa vijana wengi.
Wednesday, April 15, 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment