Lakini badala yake ameonyesha moyo wa upendo na kujali...
ameonyesha kile kiapo cha SHIDA Na RAHA hakukisema ili apigiwe vigelegele tu basi Bali ALIKUWA ANAMAANISHA
Nimeguswa sana sana....Mchango wangu wa kwanza nimeamua ku share story Kwenye page YANGU nikiamini kupitia page hii wapo watu wanaoweza kuguswa na kujitokeza kumsaidia.
Mchango wangu wa pili Nikiwa kama mkristo mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu nitamuweka Yeye pamoja Na familia yake katika maombi YANGU na mchango wangu wa mwisho nitachangia kwa chochote nilichonacho na Kwa kadri nilivyoguswa...
Ila kiukweli MABESTE MUNGU akubariki Na akusaidie upite ktk hiki kipindi kigumu ni moja Ya majaribu tu Na majaribu Yako Kwaajili yetu wanadamu...!
Mtanzania mwenzangu pita katika Page ya MABESTE soma story fupi aliyoweka na ikiwezekana Saidia kwa namna yoyote unayoweza Kutokana na utakavyo guswa .
Majaribu hayako kwa MTU mmoja Kila Mtu hujaribiwa kwa Muda wake Na kwa aina yake...!
Mungu awabariki”- Lulu aliandika kupitia ukurasa wake wa Instagram
0 comments:
Post a Comment