Pages

Subscribe:

Monday, June 29, 2015

IRENE UWOYA ATOA ONYO KWA WASANII WAUZA SURA

Baada ya  kuwa  mrembo asiye  kifani  aliyefanikiwa  Zaidi kwenye  fani , Irene  Uwoya  ameonya  wasanii wa kike  wa  Filamu wanaochipukia  kutonaswa  na mtego wa kutumia uzuri wa Sura na Maumbo yao kujimaliza  kisanii. Akizungumza na  gazeti Uwoya   alisema...  wasanii  wengi  wa  sasa  wanashindwa kufanya  kazi  kwa  sababu  wanaona  kazi  hiyo  ni  sehemu  ya  kupatia  wapenzi  wa  kiume.

Alisema  wacheza  Filamu wa  kike  huwa  wanapenda  kujirahisisha  kwa  Wanaume  na  matokeo  yake  kushindwa  kutoka  kama ilivyo kwa  wengi  wa  waanzilishi wa  sanaaa ya  uigizaji  Filamu  nchini.
Hivyo  amewataka  wasanii wa  aina  hiyo  kuacha  tabia  ya  kujilengesha  kwa  Wanaume  na  badala  yake  wajione  wapo  kazini  muda  wote.

0 comments:

Post a Comment