Ijumaa: Hongera kwa kujitosa kwenye siasa, nini kilikusukuma kuingia huko?
Wema: Nilikuwa nashauku ya kuwa mheshimiwa, hata baba yangu aliwahi kuniambia naweza hivyo nikajaribu bahati yangu.
wema (8)Ijumaa: Ukiacha marehemu baba yako, nani alikupa sapoti kubwa na ukajiona unaweza?
Wema: Namshukuru mama yangu, alinipa sapoti kubwa nikajiona naweza kwani alinitoa hofu niliyokuwa nayo.
Ijumaa: Unadhani kipi kimekuangusha kwenye uchaguzi ule?
Wema: Uchanga wangu kwenye siasa lakini naamini muda ulikuwa bado.
Ijumaa: Ingawa hukufanikiwa kupata nafasi ya ubunge umejifunza nini kupitia siasa?
Wema: Kwa kweli nimejifunza vitu vingi maana haviendani hata na umri wangu na nimepata ujasiri mkubwa. Kikubwa ukiingia kwenye siasa ujipange sana.
Ijumaa: Je, kwa hatua uliyoifikia unategemea kuendelea na siasa?
Wema: Niache? Siwezi kwani itakuwa kazi yangu, kama gari ndiyo limewaka sasa.
Ijumaa: Najua siasa ni hela hasa kipindi cha kampeni, uliwezaje kumudu gharama zote?
Wema: Ni rahisi sana ukiwa na watu wanaokupenda, walijitokeza watu kunichangia kwa ajili ya kuhakikisha nafanikiwa. Siwezi kuwataja lakini nawashukuru sana.
Ijumaa: Tulipata habari kwamba baada ya kushindwa uliangua kilio, kwa nini?
Wema: Unajua unapoenda kufanya kitu lazima una matumaini japo kuna kushindwa lakini kushinda ndiyo lengo sasa usipofanikisha lazima roho inauma.
Ijumaa: Ulijisikiaje ulipokuta nyomi la watu wakikusubiri kwa ajili ya kukupokea wakati hukuwa umeshinda?
Wema: Niliamini nina watu wengi ambao wananipenda na nilijifunza mengi kupitia ujio wao, pia walinitia moyo wa kuendelea na siasa.
Ijumaa: Kuna madai kuwa baada ya kushindwa una mpango wa kuhamia Ukawa, hilo unalizungumziaje?
Wema: Ninachojua watu wa Ukawa wamenitafuta na ilikuwa tukutane jana (Jumatatu) ila tutakutana Jumatano (juzi), nikijua wanachoniitia ndiyo nitafanya uamuzi.
Ijumaa: Baada ya kuingia kwenye mambo ya siasa tumtegemee Wema wa aina gani?
Wema: Mtarajieni Wema wa tofauti na yule mliyemzoea, mambo ya skendoskendo hayatakuwa na nafasi kwenye maisha yangu.
0 comments:
Post a Comment