Monday, July 25, 2016
TRUBADOUR AWACHANA MAKAVU ROMA, BAGHDAD NA NAY KWENYE WIMBO WAKE HEWA
Rapper Trubadour amesababisha mjadala mkubwa mtandaoni kwenye jamii ya Hip Hop ya Tanzania baada ya kuachia wimbo wake ‘Hewa’ ambamo ndani yake amewachana rappers kibao wakiwemo Roma, Baghdad na Nay wa Mitego.
“Baada ya kutoa wimbo wangu wa mpya wa HEWA, kumekuwa na maneno ya mitandaoni kwa wasanii wanaohisi kuzungumziwa. Nilichogundua ni kuwa wasanii wengi wa hip hop bongo wana uelewa finyu kuhusu...
lugha ya ufananishi,” ameiambia Bongo5.
“ Kwasababu kila nilichoongea kina maana zaidi ya moja. Vitu ninavyoweza kuweka sawa ni kuwa nimemzungumzia ROMA kama msanii na kama mji uliopo Italia. ROMA msanii ni Hewa kwa sababu ni msanii mwenye ujumbe wa uongo,” anasema.
“Kwa mfano amewahi kusema ‘pesa kweli mwanaharamu ilimponza mpaka Petro’ ukweli ni kwamba pesa haijawahi kumponza Petro bali Yuda. Pili amewahi sema ‘nasimama kama kanisa la KKT’ hakuna kanisa la KKT bali KKKT kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania. Simply Roma ana uwezo mdogo,” amesisitiza.
“Msanii kama Baghdad kwanza haeleweki anachofanya na yupo mbelembele kwa kila kitu ndio maana ya HEWA kwake. So anatakiwa kuwa competent kwenye vitu anavyofanya.”
“NAY WA MITEGO kisanaa simjui, Gigy Money anafanya mchezo na ajira za watu so akiendelea wengine tutaacha ndio maana katajwa. Wengine wote wanaohisi kutajwa wasikilize vizuri watagundua kila kilichosemwa ni lugha ya picha kina maana nyingine.”
Labels:
HABARI & UDAKU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment