Wanamuziki wawili maarufu nchini Ali Kiba na Baraka Da Prince
wanaosimamiwa na lebo ya Rockstar 4000 jana Julai 20, 2016 walivamiwa na
majambazi saa tatu usiku kwa saa za Afrika Mashariki wakiwa safarini
nchini Afrika Kusini.
Managementi inayowasimamia wasanii hao ya Rockstar 4000 imesema wasanii
hao walivamiwa wakiwa kwenye kikao cha mikakati ya kuzungumzia safari
yao nchini humo watakakokaa kwa...
muda wa siku saba.
Chanzo hicho kimesema majambazi hao walikuwa na silaha za moto (bunduki).
Miongoni mwa vitu walivyoibiwa ni pamoja na simu zao za mkononi ambapo
majambazi hao wakati wote wa tukio waliwanyooshea bunduki kina Ali Kiba
kuwatisha zaidi na bila kutaka kupoteza muda.
Baraka Da Prince na Ali Kiba wote ni wazima wa afya na hawakudhurika kwenye hilo tukio. Pamoja na tukio hili kutokea, wasanii hao hawatorudi nchini bali wataendelea na mipango yao iliyowapeleka nchini humo.
Thursday, July 21, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment