Pages

Subscribe:

Friday, November 11, 2016

HAYA NDIYO MATOKEO YA KUFUZU FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA MECHI ZILIZO PIGWA HUKO AMERICA KUSINI


mmg_4106
Timu ya soka ya wanaume ya Brazil ya Neymar, imefanikiwa kuifunga timu ya Argentina ya Messi mabao 3-0 kwenye mchezo wa kufuzu kucheza kombe la dunia nchini Urusi mwaka 2018. 

Mchezo huo ulifanyika kwenye uwanja wa Belo Horizonte, Brazil na wenyeji kufanikiwa kuibuka na mabao hayo kupitia kwa wachezaji wake Philippe Coutinho aliyefunga goli la kwanza kwenye dakika ya 25, Neymar aliyefunga dakika ya...
45 na goli la mwisho lilifungwa dakika ya 59 na Paulinho.

Ushindi huo umeifanya timu hiyo ya Brazil kuongoza kundi la timu za bara la Amerika ya Kusini ikiwa na pointi 24 kati ya michezo 11 waliocheza mpaka sasa huku Argentina ikibakia kwenye nafasi yake ya sita ikiwa na pointi 16. Matokeo mengine ya michezo ya kuwania kufuzu kombe la dunia iliyochezwa alfajiri hii kwenye bara hilo ni:
Uruguay 2 – 1 Ecuador
Paraguay 1 – 4 Peru
Venezuela 5 – 0 Bolivia
Colombia 0 – 0 Chile

0 comments:

Post a Comment