Pages

Subscribe:

Wednesday, November 9, 2016

MENEJA WA DJ VAN: TANZANIA NA MOROCCO ZITASHIRIKIANA KIMUZIKI


b760a28e-12f6-4cd0-9a0c-dbf168647b6b
Meneja wa Dj maarufu wa nchini Morocco, DJ Van, amesema ushirikiano ulioanzishwa
kati ya nchi yake na Tanzania baada ya mfalme wao Mohammed V kuja nchini hivi
karibuni, una nafasi nzuri kwa wasanii wa nchi hizo kushirikiana pia.

Morocco ndio nchi inayoongoza kwa kuwa na wasanii wakubwa na waliofanikiwa zaidi katika nchi za Kaskazini mwa Afrika. Meneja huyo, Janatte Haddadi, amedai...
kuwa baada ya kusikia taarifa kuwa wananchi wa Morocco wanaweza kuja Tanzania bila visa, walifurahi na kwamba watakuja kwa wingi.

“Sanaa na utamaduni huwaweka watu karibu, hivyo kama tutaweza kufanya kitu na Diamond bila shaka, itafungua connection kati ya Tanzania na Morocco,” alisema Haddadi. “Itafungua milango kwa watu katika nchi yenu na kwa watu wangu pia,” ameongeza.
01bb44ae-343a-402f-8169-f5b5b278ab62
Janatte Haddadi (kulia) akiwa na wenzake kutoka nchini Morocco kwenye tuzo za 
Afrima, Haddadi amedai kuwa ni muhimu sasa kukawepo na ukaribu wa kumuziki 
katika nchi za Afrika Kaskazini na zingine za Kusini, Mashariki na Magharibi.

0 comments:

Post a Comment