Pages

Subscribe:

Thursday, November 10, 2016

MKOLONI ATOA SABABU YA WASANII KUWA WENGI KWENYE JUKWAA MOJA


Wiki iliyopita Mtayarishaji mkongwe wa Muziki wa Bongo Fleva nchini kutoka studio za MJ Records Master J, alikuwa kwenye kipindi cha redio moja nchini akizungumzia ongezeko la maproducer hapa
nchini. 


Lakini pia hakuishia hapo alizungumzia ishu za Album hususani kwa wasanii wa Tanzania na kusema kuwa mara yake ya mwisho kutengeneza Album ni mwaka 2008 na kwa upande wa...
Album iliyomuingizia Pesa ni Album ya Wagosi wa Kaya walioitoa miaka ya 2000.

Sasa Leo Mkoloni kutoka kwenye Kundi la Wagosi wa kaya lenye maskani yake jijini Tanga alikuwa mgeni kwenye kipindi hicho na kuzungumzia ishu za Album kwa wasanii wa Bongo fleva na kusema kwamba.. 

“Hauwezi kuwa msanii mkubwa Duniani kama hauna hata Kanda mseto (mixtape) kwani Duniani kote wasanii wakubwa wana Album ndiyo maana wanajulikana”
Aliongeza kwa kusema wasanii wengi wa Bongo wanasema album haziuzi wakati hawajawahi hata kurekodi Album na ndiyo hao wanaojazana kwenye show kwa kuwa wote wana ngoma chache hawana Album, Utakuta msanii anaimba Nyimbo mbili tu jukwaani halafu anashuka sasa wasanii kama hao
lazima wang’ang’ane na show.


“Wanaolalamika Album haziuzi wengine hata hawajawahi kurekodi ama kutoa Album, wasanii wanajazana kwenye show kwa kuwa wote wana ngoma chache hawana Album, na matokeo ya kukosa album msanii anaenda kwenye show anaimba nyimbo mbili tu…” 

Pia aliendelea kwa kuuliza “Hivi msanii unawezaje kufika Level za kimataifa wakati huna hata Album?”
Mkoloni yeye bado anaamini album ni muhimu kwa msanii yeyote Duniani sio Tanzania tu kwani watu wanatoa album kwa ajili ya heshima sio kwa ajili ya mauzo tu, kwani huwezi kuwa msanii wa kimataifa halafu hauna hata Album moja.
Kwa sasa Mkoloni yupo na biashara zake lakini pia yupo mbioni kutoa Mixtape yake.

0 comments:

Post a Comment