Wednesday, November 2, 2016
PROFFESOR JAY ATOA KAULI HII MPYA JUU YA SINGELI
Mh Mbunge na Rapper kutoka nchini Tanzania, proffesor Jay amesema inampasa kuwasaidia wanamuziki wa singeli kwa kuwa ni muziki unao tangaza utamaduni wa nyumbani.
Siku zinazidi sogea na muziki huu wa Singeli unazidi shika nafasi, huku wasanii na wadau mbalimbali wakitolea maoni juu ya muziki huu wa singeli huku kwa upande wa pili kukiwa na...
kundi la wasanii wakidai huu ni muziki wa kupita yani hauta dumu na wengine kutaja ni muziki wa kihuni.
Imekuwa tofauti kwa Rapper Professor Jay, ambae amezungumza na shirika la utangazaji la BBC nakubainisha kauli yenye nishati ya namna yake kwa kusema
”kwa nini watu wafe na mazingira magumu wakati wana vipaji? alihoji.. ntawasapoti kwa kuwa muziki wa singeli unatangaza utamaduni wa nyumbani”
Hiyo ndio imani ya msanii mkongwe nchini Professor Jay na kauli yake ya ‘Why These people are dying hungry but they have talent’ aliyo isema Professor Jay ndio inaipa mashiko kauli yake ya hapo mwanzo.
Labels:
HABARI & UDAKU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment