Imekuwa tofauti kwa mastaa mbalimbli hapa nchini kusherehekea siku zao za kuzaliwa kwa kufanya jambo au mambo tofauti tofauti.
kutoka Mji kasoro Bahari Morogoro, anapotokea rapa Stamina ambae Leo ana sherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kumkumbuka marehemu mama yake mzazi kwa...
kusafisha kaburi la mama yake mzazi lililopo kwenye makaburi ya kora mjini morogoro.
Leo kwenye ukurasa wake wa Instagram aliposti picha akiwa kwenye Kaburi la mama yake na kuandika..
“Mungu ni mwema sana asante kwa kunifikisha siku ya leo nimeona nitembelee kusali kwenye kaburi la marehemu mama yangu aliyenizaa siku kama ya leo (R.I.P MAMA) Ahsanteni mashabiki zangu wote/madj wote/presenterz wote rafiki ndugu na wadau wa hii sanaa kwa sapoti yenu. Happpy Birthday to me.”



Follow on Instagram
0 comments:
Post a Comment