Wednesday, May 31, 2017
MRISHO MPOTO ASEMA NENO KUHUSU MZEE ALIYECHORA NEMBO YA TAIFA LA TANZANIA
Msanii wa muziki wa kughani nchini Tanzania, Mrisho Mpoto amesikitishwa na kifo cha Mzee Francis Kanyasu aliyechora Nembo ya Taifa na kusema anatamani siku zirudi nyuma ili aweze kuongea naye tena.
Mpoto amefunguka hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kudai Mzee huyo alishawahi kumsaidia kumpa wazo la kufanya video ya wimbo wake wa ‘Njoo Ichukue’.
“Hii ni taarifa ya kunisikitisha sana kwenye maisha yangu ya muziki, nakumbuka kabla ya...
kutoa wimbo wa ‘Sizonje’ nyuma yake nilitoa ‘Njoo nichukue’ huyu Mzee alikuja ofisini kwangu kuniambia maneno mazito sana kwamba anapenda kazi yangu na alinitabiria mambo mengi mazuri kwenye safari yangu ya maisha nanukuu YACHUKULIE MANENO HAYA NI YA CHIZI KAONGEA” aliandika Mpoto.
Aidha Mpoto aliendelea kusema kuwa “Ombi lake lilikuwa moja tu alitamani kufanya kazi na mimi, ofisi nzima ikamchukulia kama mzee aliyechanganyikiwa wakataka kumfukuza, mlinzi wetu wa ofisi akasema msimpuuze mpeni nafasi, tulipompa nafasi ndiyo akatoa wazo la video ya wimbo wa ‘Njoo uichukue’ iweje, na akasema yule mzee Mshuba kikongwe muuza bangi ataigiza yeye mwenyewe tulicheka Sana maana wazo lake lilikua zuri na liliungwa mkono na ‘Director’ Adamu Juma”
Pamoja na hayo Mpoto amesema baada ya kupata taarifa ya kifo ndipo alipokuja kugundua kuwa Mzee Francis anamfahamu vizuri.
“Baada ya kuangalia kwa makini kumbe ndiyo yule mzee aliyefariki leo mchora Nembo ya Taifa, natamani siku zirudi nyuma niongee naye tena, roho imeniuma sana kwa kweli sijui hata nifanye, nini kibaya zaidi baada ya ‘shooting’
alitutoroka hata hatukujua tutampataje”.alisisitiza Mpoto
Labels:
HABARI & UDAKU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment