Bweni la wasichana wa shule ya sekondari Kipoke mkoani Mbeya
limeteketea kwa moto na kusababisha uharibifu mkubwa huku wanafunzi
wawili wakijeruhiwa.
“Ni bweni la wasichana kidato cha pili limeungua moto
ambapo mpaka sasa hatujajua chanzo chake kama ni umeme au ni wanafunzi
wenyewe tumeshindwa kufahamu.
Tumefanya jitihada za kunusuru vitu vya wanafunzi na wao wenyewe lakini tumefanikiwa kwa kiasi kidogo kutokana na baadhi ya vitu ikiwemo magodoro na vitanda 68 kuteketea na moto”, amesema Mwanyila.
Pamoja na hayo, Mwanyila ameendelea kwa kusema “ni vijana watano pekee waliojeruhiwa kidogo na moto huo baada ya wao kusaidia kukata bati ili moto usiweze kuenea katika maeneo mengine ya bweni”.
Kwa upande mwingine, Mwanyila amesema bado hawajaweza kujuwa tathimini kamili ya mali za shule zilizoweza kuteketea na moto kutokana bado hawatulia tokea ajali hiyo ya moto ilipoanza.

Follow on Instagram
0 comments:
Post a Comment