Msanii wa muziki Bongo, Vanessa Mdee amesema muziki wa Afrika Mashariki
haupewi nafasi kubwa nchini Nigeria kama inavyokuwa ikitazamiwa.
Muimbaji huyo ambaye yupo nchini humo kwa ajili ya kutangaza albamu yake
‘Money Mondays’ ameiambia Clouds Fm kuwa katika moja club alizopita
alikuta ngoma zinazochezwa ni ya Patoranking na Diamond ‘Love You Die’
na ile...
aliyoshirikiana na Reekado ‘Move’.
“Hapa Nigeria haupo kabisa muziki wa Tanzania, haupo kwa nguvu ambayo
unatakiwa kuwepo kwa sababu tunaelewa muziki wetu ni mkali, wasaniii
wetu ni wakali. Kidogo wanauzito wa kupokea muziki wa East Africa, jana
nilikuwa club nilisikia nyimbo za Tanzania ambazo zinapigwa ni ile
Diamond na Patoranking na ya kwangu na Reekado ‘Move’ hakuna nyimbo
nyingine inapigwa hata ya Afrika Mashariki,” amesema.
Pia Vanessa amesema si kwamba hawatambui muziki kutoka Afrika Mashariki
ni mzuri ila wameamua kuupa kipaumbele muziki wao na kutokana na idadi
kuwa wasanii walionao inakuwa ni vigumu kwa muziki kutoka sehemu
nyingine kupata nafasi.
Monday, February 5, 2018
VANESSA MDEE: MIMI NA DIAMOND NDIYO WASANII WA AFRIKA MASHARIKI TUNAO SIKIKA NIGERIA
Labels:
HABARI & UDAKU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment