mashabiki wa Kiba wameitabiria makubwa ngoma hiyo licha ya kwamba bado hawajaisikia na kusema kuwa huenda unaweza kuwa wimbo wa Taifa tena kwa namna utakavyotamba na kupokelewa mitaani.
Jumaa_salim "Hope itakuwa nyimbo ya taifa kama zilizopita, mwenye kipaji ni kama perfume lazima harufu isikike. Ali Kiba unajua"
Baby_anney "Jamani can't wait maana napenda sana kazi zako hamna mfano wake my favorite @officialalikiba"
Frank Mugasa "Yani naisibiri kwa hamu ngoma iyo inipoze machungu ya kufungwa na monaco"
Moja ya mstari ambao unapatikana katika kazi mpya ya Alikiba unasema "Kama mapenzi ghorofa yamejaa Kariakoo"
Ali kiba aliachia nyimbo zake mbili Kimasomaso na Mwana tarehe 25/July/2014 baada ya kimya cha muda mrefu na baadae kuna nyimbo mbili zilitoka ambazo kwa mujibu wa Ali Kiba alidai kuwa hakuzitoa bali zimevuja ila alidai kuwa atakachokifanya ni kuzifanya nyimbo hizo ziwe katika kiwango kizuri ili ziweze wafikia mashabiki kwa ubora zaidi na ziweze kuchezwa katika vituo mbalimbali vya redio.
0 comments:
Post a Comment