skip to main |
skip to sidebar
HIKI NDIYO CHANZO KILICHO PELEKEA BABA MZAZI WA DULLY SYKES KUFARIKI
Marehemu Mzee Abby Sykes ambaye ni Baba mzazi wa mwimbaji wa Bongo Fleva
Prince Dullysykes, alifariki saa 8 mchana February 15 2015 akiwa
hospitali ya taifa Muhimbili kwa ajili ya kupatiwa matibabu. Dullysykes ameongea na millardayo.com ikiwa ni pamoja na kuelezea kitu
kilichosababisha umauti wa baba yake ambapo ameanza kwa kusema..."Mzee alikua ana vidonda katika miguu na ndiyo chanzo kikubwa, sumu
ikasambaa ikasababisha kifo chake, vidonda vilishindwa kupona kwa ajili
ya moshi wa sigara ila zaidi hakuwa na tatizo jingine lolote manake baba
yangu alikua strong"
‘Alianza kuugua vidonda miezi minne iliyopita, miezi miwili alikua
anavumilia tu lakini miezi miwili ya mwishoni ndiyo vilizidi kumsumbua,
mazishi tunategemea kuyafanya February 16 2015 saa kumi jioni kwenye
makaburi ya Kisutu lakini safari ya kwenda msikitini tutaanza saa 7
mchana‘ – Dully.
0 comments:
Post a Comment