skip to main |
skip to sidebar
HATIMAYE MAMA MZAZI WA DIAMOND AREJEA KUTOKA INDIA KWENYE MATIBABU
Mungu ni mkubwa :Mama mzazi wa Supastaa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul
‘Diamond Platnumz’, Sanura Kassim ‘Sandra’, amerejeshwa Bongo kutoka
India ambapo afya yake imetengemaa. Habari kutoka chanzo cha kuaminika ndani ya familia ya jamaa huyo, kimesema kwamba... tayari Sandra amesharejea katika hali yake ya kawaida na
ndiyo maana akarudi Bongo baada ya kulazwa hospitalini nchini India kwa
kusumbuliwa na ugonjwa wa kupooza.
Mwanafamilia huyo alisema kwamba, Diamond na mama yake walirejea nchini
wikiendi iliyopita baada ya kufanyiwa matibabu ya kina na madaktari
kujiridhisha kwa hali ya juu dhidi ya afya yake ambapo waligundua hali
aliyonayo kwa sasa imetengemaa hivyo wakamruhusu kurejea kuungana na
familia yake.
Habari zilieleza kuwa kwa sasa bimkubwa huyo yupo fiti na anaendelea na
mazoezi ya kawaida huku akimalizia dawa alizopewa na wataalam hao wa
afya.
0 comments:
Post a Comment