Pages

Subscribe:

Monday, March 30, 2015

VIDEO YA DIAMOND YAWAKOSHA AFRIKA MAGHARIBI NA KUSINI

Video hiyo inaonesha utamaduni wa mswahili wa pwani ambaye amerithi mambo mengi kutoka kwa waarabu. Hivi ni vitu ambavyo Afrika na dunia nzima imevisoma kwenye historia ya ukoloni. Kupitia video na wimbo wake, Diamond amewapa mashabiki wa muziki wa Nigeria, Ghana, Afrika Kusini na nchini zingine nje ya Afrika Mashariki... picha halisi ya maisha ya mswahili.

Taarab na mduara ni nyimbo zenye asili ya Tanzania na hivyo wimbo kama ‘Nasema Nawe’ inawakilisha kile tunachoweza kusema kwa kujigamba kuwa ni muziki wa Tanzania. Kitendo cha kumuongeza Khadija Kopa, malkia wa mipasho nchini, kimeuongezea thamani kubwa sana wimbo huo.

Nisisahau kusema kuwa Khadija Kopa na Hanscana wamewekwa kwenye sehemu ambayo sasa jicho la Afrika linawaona.

Hivi ni vitu vigeni kwa nchini kama Nigeria na Ghana. Hivi ni vitu ambavyo wasanii wao hawawapi kwasababu sio utamaduni wao. Ndio maana pamoja na kutoelewa Kiswahili, bado wamevutiwa na video na wimbo huo kwasababu wanasikia ladha mpya na kuona picha za tofauti.

“I dont understand a single word,but Diamond is honestly as his name says. Loyal fan from Namibia. #teamdiamond,” ameandika Rauha Vroutjie.

Jana jina la Diamond lilifanikiwa kushika namba moja kwenye trend topics za kwenye mtandao wa Twitter masaa machache tu baada ya kuachia video hiyo. Kwa msanii wa Tanzania kutrend Lagos, Nigeria si kitu cha kawaida, ni kikubwa.

Diamond amevuka hatua ya kuwa msanii maarufu Tanzania peke yake na kuwa msanii maarufu Afrika. Akishuka Luanda, Angola ama Gaborone, Botswana, hakuna shaka wengi watakuwa wanaifahamu sura yake.

Sehemu alipofikia ana uwezo wa kufanya wimbo wowote na Afrika ikamuelewa. Kutengeneza wimbo wenye vionjo vya Tanzania ni uamuzi mzuri zaidi alioufanya.

Kwahiyo msisitizo ninaopenda kuutoa hapa ni kwamba hatuwezi kuwashtua wanaijeria ambao kwa sasa ndio wameushikilia muziki wa Afrika, kama tukiiga muziki wao na kuwapa ladha ile ile wanayopewa na wasanii wao. Hawawezi kushtuka!

Hebu fikiria mfano huu. Kama wewe ni mkazi wa Bukoba na ukaja kumsalimia ndugu yako wa Dar es Salaam halafu chakula pekee atakachokupa kikawa ni ndizi, utajisikiaje? Umeziacha ndizi pomoni Bukoba halafu unakuja Dar unapikiwa ndizi tena? Tafakari.

Kwahiyo wasanii wanaopata bahati ya kuwashirikisha wasanii wakubwa wa Nigeria au Afrika Kusini, ili collabo zao zionekane za maana wanatakiwa kutengeneza nyimbo zenye ladha ya Tanzania ili kuwapa wapenzi wa muziki huo muziki tofauti.

Kwa wasanii ambao wamepata bahati ya kuwa na majina makubwa, kama wanataka kuchukuliwa serious, wahakikishe kama hawatengenezi nyimbo zenye mahadhi ya dunia (universal genres) ambazo ni pamoja na Hip Hop, R&B ama Pop, basi watengeneze nyimbo zenye ladha halisi ya Tanzania, yaani Bongo Flava.

Mtanzania akifanya Kwaito au muziki wa Naija nahisi kama hatofika popote.

0 comments:

Post a Comment