Pages

Subscribe:

Tuesday, March 17, 2015

AUNTY EZEKIEL: WEMA NA KAJALA IPO SIKU WATAKUJA KUJUTA

Staa anayefanya vizuri kwenye tasnia ya filamu Bongo, Aunt Ezekiel amefunguka kuwa anatamani aone mastaa wawili ambao wana bifu kali, Wema Sepetu na Kajala Masanja wanamaliza tofauti zao kwani maisha ni mafupi.
 

 Akizungumza, Aunt alisema kati ya mabifu ambayo angependa yaishe ni la Wema na Kajala kwani wapo wasanii wamefariki dunia wakiwa na bifu huku wale waliobaki ambao walikuwa na mabifu nao wakitamani waamke walau mara moja wamalize tofauti zao lakini haikuwezekana...
“Jamani maisha haya ni mafupi sana na tunatakiwa kujifunza kutoka kwa wenzetu tuliokuwa nao lakini sasa hivi hawapo tena, natamani sana Wema na Kajala wamalize tofauti zao  kwani ipo siku watakuja kujuta siku ambayo mmoja wao atakapokuwa hayupo japo siwaombei ila hilo ndilo tamanio langu kuwaona wakizungumza,” alisema Aunt

0 comments:

Post a Comment