skip to main |
skip to sidebar
KINGWENDU AMSAMEHE ALIYE MBAKA MKEWE
MSANII wa vichekesho Bongo, Rashidi Mwinshehe ‘Kingwendu’ amefunguka
kwamba japokuwa alipata maumivu ya moyo baada ya jirani yake kumbaka
mkewe, Mama Maua ameamua kumsamehe. Kingwendu alisema mara nyingi mkewe alikuwa... Akimwambia kuhusu jirani
huyo kumtongoza lakini akawa anamkatalia lakini siku hiyo alimvizia na
kutimiza azma yake ambapo baada ya hapo alikimbia mpaka leo hajarudi ila
amemsamehe kwa kuwa hata Mungu anasamehe mara nyingi.
“Mimi nasali sana hivyo nimeamua kumsamehe huyo jamaa kwa sababu hata
Mungu huwa anatusamehe mara nyingi, alishawahi kumtuma dada yake aje
kuniomba msamaha maana yeye alikimbilia huko Kilwa na mimi na mke wangu
tuko vizuri ninampenda sana na najua halikuwa kusudi lake ila mwanaume
huyo alimsumbua kwa muda mrefu,” alisema Kingwendu.
0 comments:
Post a Comment