Staa wa Bongo Fleva,Nay Wa Mitego hivi karibuni aliweka
wazi majibu yake baada ya kupima UKIMWI kupitia account yake ya
Instagram na kwamba alikuwa yupo safi yaani(Negative).
Alipoulizwa sababu ya kupima ngoma alisema kuwa alikuwa
akiumwa ugonjwa wa...
Malaria na alikuwa hajaugua kwa muda mrefu na
alipokwenda hospitali ilibidi apime na ngoma ingawa ni kawaida yake
kupima mara kwa mara.
‘’Nilipima baada ya kuumwa Malaria lakini huwa ni
kawaida ya kupima ngoma hata mke wangu(Siwema) alipokuwa mjamzito
tulikwenda pamoja kupima hospitali,"alisema Nay.
Alipoulizwa kama tangu alipoanza uhusiano na mke wake Siwema alishawahi kuchepuka alisema kuwa ni kweli alishawahi kufanya hivyo ila hawezi kusema ni mara ngapi ili kunusuru ‘ndoa’ yake.
Alipoulizwa kama tangu alipoanza uhusiano na mke wake Siwema alishawahi kuchepuka alisema kuwa ni kweli alishawahi kufanya hivyo ila hawezi kusema ni mara ngapi ili kunusuru ‘ndoa’ yake.
"Unajua ni mambo ya ujana, ni kweli nilishawahi
kuchepuka lakini siwezi kusema ni mara ngapi si unajua mama watoto
anaweza kukasirika? Lakini nilikuwa makini sana na namwomba sana msamaha
mke wangu na sitegemei kuchepuka tena,’’alisema Nay.
0 comments:
Post a Comment