Kundi la Wanamgambo wa Al-Shabaab wa nchini Somalia, Leo tarehe 4/4/2015
asubuhi na mapema, wametoa TAMKO lao kuhusiana na mfululizo wa matukio
ya kushambulia nchini Kenya na sababu za wao kufanya hivyo, huku
wakieleza dhamira yao ya kuendelea kufanya matukio zaidi iwapo madai yao
hayatatimizwa na Serikali ya nchi hiyo.
Madai Makuu ya msingi ya Al-Shabaab waliyoainisha kwenye Tamko hilo,
wamesema Serikali ya Kenya imekuwa... ikiwaua Waislamu kwenye Ukanda wa
Afrika Mashariki, huku wakitolea mfano wa historia ya Mauaji ya kutisha
ya Waislamu yaliyotokea katika miji ya Wagalla na Garissa ambapo wamedai
zaidi ya Maelfu ya Waislamu waliuawa na kuacha makovu yasiyofutika kwa
ndugu na jamaa wa wahanga hao.
Pia, wameshutumu Majeshi ya Kenya kwamba yamekuwa yakiwafanyia vitendo
vibaya raia wa Kiislamu wa Somalia vikiwemo ubakaji, mauaji na
udhalilishaji wa wanawake wa Kiislamu kwa 'baraka' za serikali ya Kenya.
Zaidi katika tamko hilo, Wanamgambo hao wamedai kwamba iwapo Serikali ya
Kenya haitaacha kuwatendea unyama Waislamu, basi wataendelea na
mashambulizi yasokwisha!
0 comments:
Post a Comment