skip to main |
skip to sidebar
Penny: USISTA DUU UTATUMALIZA WASICHANA WA BONGO
Aliyekuwa mtangazaji wa kituo cha redio cha Efm, Peniel Mungilwa ‘Penny’
amefunguka kuwa tabia ya baadhi ya wasichana mastaa kujiona masista duu
itawamaliza kwa sababu watajikuta uzee unawakabili bila kuwa na ndoa. Akizungumza na mwandishi, Penny alisema mastaa wengi wanapenda kujiona
ni matawi ya juu na kufikia hatua ya... kudharau watu wengine kiasi kwamba
hata wenye mapenzi ya dhati kwao hujikuta wakijiweka pembeni hivyo
kuwafanya ‘kuchina’ wakati wakitafuta ndoa.
“Unajua kuna vitabia fulani hivi mastaa tunavyo, ya kisista duu ambayo
inatufanya tuchine, maana wengi si wanatuogopa wakidhani sisi ni matawi
ya juu wakati ni wa kawaida sana,” alisema Penny.
0 comments:
Post a Comment