Msanii wa Bongofleva ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake wa
'Ganda la Ndizi' Nuh Mziwanda akiwa na mchumba wake Shilole amefunguka
na kusema watu wengi walimshauri mpenzi wake huyo amuache. Nuh amesema watu walimpatia ushauri huo Shilole, baada ya hivi
karibuni kusambazwa sauti yake katika mitandao ya jamii akisikika
kumtaka kimapenzi...
msanii wa Bongo Movie Wema Sepetu, mazungumzo yao
yalikuwa yamerekodiwa kwa njia ya simu na kusambazwa na mtu
asiyejulikana.
Nuh Mziwanda amesema baada ya sauti hiyo kusambazwa watu wengi
walikuwa wakimpigia simu Shilole na kumshauri aachane naye lakini
anamshukuru Mungu, Shilole hajaweza kuwasikiliza na wanaendelea poa na
maisha yao kama wapenzi na kudai Mungu ana kusudio lake kufanya
waendelee kuwa pamoja.
"Wengi mlishauri aachane na mimi, ila Mungu ana kusudio lake kufanya
tuendelee kuwa pamoja na nampenda sana Shishi wangu na sifikirii
kumuacha," alisema Nuh Mziwanda.
Baada ya kauli hiyo ya Nuh Mziwanda mashabiki wake katika mitandao ya
jamii walimbadilikia na kusema kuwa anapenda sana mteremko na
kutafutiwa ndiyo maana anahangaika na watu ambao wamemzidi umri, huku
wengine wakionyesha kutopenda mambo yake ya ndani anavyoanika katika
mitandao ya kijamii hususani kuhusu mapenzi yake na mchumba wake.
0 comments:
Post a Comment