Kwenye
sauti utamkuta, Elias Chimenya aliyefungwa kwa mauaji, gitaa la besi, jambazi,
Stefano Nyerenda huku askari, Thomas Binamo akiwa mmoja wa waandishi wa nyimbo
za kundi hili.
Bendi
ya Zomba Prison Project ya Malawi itawania tuzo za Grammy zitakazotolewa mwezi
ujao nchini Marekani. Albamu yao yenye nyimbo 20, ‘I Have No Everything Here’
ilitajwa kuwania kipengele cha Best...
World Music Album kwenye tuzo hizo.
Kundi
hilo lilianzishwa mwaka 2013 kwenye gereza lenye ulinzi mkali la Zomba baada ya
mtayarishaji wa muziki wa Marekani, Ian Brennan alipotumia wiki mbili
kutengeneza albamu hiyo na wafungwa 60.
Elias
Chimenya, 46, anayetumikia kifungo cha maisha kwa kumuua mtu kwenye ugomvi
miaka ya 1980, aliandika wimbo uitwao ‘Jealous Neighbour.’
Amesema
muziki umemfanya awe mtulivu na kuzoea maisha ya jela. “Ninaamini sitafia jela,
badala yake nitaachiwa ili nikaendelea na muziki nje,” aliliambia shirika la
AFP.
Wamesema
kutajwa kwenye tuzo za Grammy ni kitu ambacho hawakukitegemea.
“Tumeshangazwa
kwasababu hatukutegemea wafungwa kutajwa,” alisema Nyerenda, 34 anayetarajia
kutoka jela mwakani baada ya kutumikia kifungo cha miaka 10 jela kwa kufanya
tukio la ujambazi.
0 comments:
Post a Comment