Pages

Subscribe:

Thursday, July 7, 2016

STAMINA: YOUNG DEE ARUDI, ASIRUDI MTU CHEE WE DON'T CARE


Stamina ameijibu kauli ya Young Dee kuwa suala la kuwaomba msamaha yeye na Country Boy ili arudi kwenye kundi la Mtu Chee ‘halimake sense’ kwa kudai kuwa in fact wao hata hawashtui.
 
Akiongea, Stamina amesema yeye na Country Boy wamekuwa mastaa kama wasanii wanaojitegemea na sio kupitia Mtu Chee na kwamba kutokuwepo kwa Young Dee...
hakuathiri chochote kwenye kundi hilo.

Amedai kuwa wao wana utofauti mkubwa na yeye kwakuwa kila wanachokifanya wamekuwa wakijilipia wenyewe, tofauti na Young Dee aliye chini ya uongozi wa MDB hivyo hawapo kwenye ligi moja hata kidogo. “Mtu kama mimi unadhani ninaweza nikababaishwa na sentensi kama hiyo ya yeye kutorudi kwenye group?” amehoji Stamina.


“Mimi ni mwanajeshi ambaye ni jeshi la mtu mmoja sifungamani na mtu na wala sitegemei usaidizi wa mtu mimi, mimi naweza nikasurvive mwenyewe na mambo yangu yakaenda vizuri tu. Kwahiyo kauli yake yeye arudi, asirudi sisi walaa, kwanza habari yake nimeiona Bongo5, nisingeiona walaa, kwanza simpigiagi simu, yaani sio mwana kiufupi,anajua mwenyewe mistake zake anazofanyaga. Kwasababu sasa hivi anaona amerudi sehemu ile ile, anarudi kwenye yale matapishi aliyokuwa amekula mara ya kwanza, ameona kuwa watu wamekubali kumsaidia tena it’s okay. Halafu mimi si selfish aisee, sababu huyu huyu siku kadhaa tu zilizopita tulikuwa tunaishi naye kitaa vizuri tu na tulikuwa na mipango ya kufanya naye kazi lakini mimi watu wenye dharau sio wanangu kabisa,” amesisitiza Stamina.


“Kwahiyo yeye kwa kauli yake hiyo yeye hajamtetemesha mtu yeyote, nikijisikia kufanya kazi na Country Boy nitafanya naye kama yeye sio tena group. Tena kwa taarifa kama hizi nafurahi kwasababu pia naona group life na kila mtu afanye vitu vyake sababu mimi muziki wangu haufungamani na group kwahiyo I don’t care.”
“Kama jana nimeona kauli yake eti ‘haimake sense’, hell no nigga, yeye ndio hamake sense, halafu askate watu tuanze kuzungumza kauli zetu za ndani pia, kwasababu mimi battle za mdomo siwezi, ukitaka battle washa mic tubattle.”

0 comments:

Post a Comment