Pages

Subscribe:

Friday, November 18, 2016

BEN POL KUFUNGA MWAKA NA KOLABO YA KIMATAIFA

ben-pol1
Msanii wa muziki wa RnB Ben Pol baada ya kusitisha kuachia albamu yake mpya kama alivyoahidi mapema mwaka huu, anatarajia kufunga mwaka kivingine kwa kuachia kolabo na msanii wa nje. Akiongea na Bongo5 wiki hii, Ben Pol amesema baada ya kupata changamoto kadhaa na kushindwa kuachia albamu, anajipanga kuachia wimbo mpya pamoja na video.

“Albamu nitaachia mwakani kwa sababu sasa hivi watu wanataka wimbo mpya,” alisema Ben Pol “Moyo Mashine tayari imeshafanya ilichofanya kwa sasa mashabiki wanataka wimbo mwingine. Kwahiyo najipanga kushoot video ya...
nyimbo nyingine, kula kolabo moja na msanii wa Ghana na nyingine msanii wa Nigeria Chidinma, Kwahiyo hapa tunaangalia ipi tuanze kushoot video na pia kuna nyimbo zangu nimefanya mwenyewe,”

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo Moyo Mashine, ameshindwa kuachia albamu mpya kama alivyoahidi kutokana na biashara ya muziki kumkalia vibaya mwaka huu.

0 comments:

Post a Comment