Nikki wa Pili ni msanii mwenye upeo, akili nyingi, mawazo positive katika kila harakati za kimaendeleo na amekuwa akitumika vizuri katika kutoa somo kwa baadhi ya vijana ili kuhakikisha anawapa njia za kuweza kufikia malengo yao.
Ameweza kujijengea heshima na uaminifu kwa wengi kutokana na kile anacho kizungumza kuwa chenye matokeo chanya na hivyo kufanikiwa kuwaaminisha wengi kile...
anachokiamini kutokana na upeo wake.
Mapema asubuhi ya leo katika mtandao wa instagram mkali huyo aliweza kutoa somo kwa wengi baada ya kupost picha ya raisi mpya wa Marekani Donald Trump na kuandika caption flani hivi iliyotumika kama somo kuhusiana na suala zima la demokrasia.
Kwenye Insta nikki ameandika: Miaka 10 iliyopita makampuni 50 yalikuwa yana miliki 90% of america mainstream media....sasa ni makampuni 6 yana miliki mainstream media zote za america....na kwa gharama ya 41. Billion$ donald drump aliweza kununuwa airtime kubwa ndani ya miezi 8 nakuwa rais wa america........media zinajali wamiliki wake na faida zao, wananchi wanatizamwa kama wateja.....same is happen dunia nzima juzi tu tulishuhudia maswali ya wahariri....bila kusahau uchaguzi wa mwaka jana na namna media zilivyo kuwa vyombo vya propaganda...democrasia sasa ni bidhaa na itanunuliwa na wenye fedha na hii ni ulimwengu mzima....dunia inahitaji mfumo mpya
Tumeemtafuta Nikki wa Pili na kupiga nae story ili kujua ni kipi alimaanisha katika post yake ya Instagram. Nikki wa Pili amefun guka mengi zaidi kuhusiana na demokrasia na kudai kuwa siasa siku hizi imekuwa biashara na mtu huwezi kupata uongozi serikalini bila kuwa na pesa.
Nikki wa Pili ametolea mfano ushindi wa raisi mpya wa Marekani Donald Trump, na kudai kuwa Trump ametumia pesa nyingi sana kuhakikisha anapata uongozi na kilichompa nguvu Trump ni katika kuwekeza kwenye kujitangaza katika media tofauti tofauti nchini humo na mwisho wa siku kufanikiwa kutwaa kiti hicho.



Follow on Instagram
0 comments:
Post a Comment