Pages

Subscribe:

Thursday, November 17, 2016

STAMINA AFUNGUKA CHANZO CHA YOUNG KILLER KUPOTEA KWENYE RAMANI YA MUZIKI


Ni ukweli usiofichika kuwa Young killer wa sasa na wa miaka miwili iliyopita wana utofauti mkubwa, kutokana na yule wa kipindi kile alikuwa na uwezo wa kutengeneza hit na zikafanya vizuri kwa kipindi kirefu tofauti na huyu wa sasa ambaye anaonekana kushuka kimuziki kutokana na level ambazo alikuwepo zamani.

Rapper Stamina amefunguka kuwa anahisi kitendo cha Young Killer kuondoka katika lebo ya Mona Gangstar ni sababu kubwa iliyomfanya mkali huyo kufeli kimuziki, Akiongea Stamina amedai kuwa ngoma za sasa za Young Killer zinashindwa...
kuhit kama zile za mwanzo kutokana na sasa Young Killer hayupo na Mona Gangstar akihisi kwamba Mona alikuwa akimshape Young Killer.

“Young Killer kwasasa anatakiwa kuwa positive, anatakiwa kuangalia alikosea wapi. Laana ni mbaya sana, hamna laana mbaya kama ya mdomo. Me nadhani hata kama mtu uliachana nae for good lakini kama yeye bado anakitu moyoni ambacho kinamzuia kufungua moyo wake kwako, hiyo huwa ni mbaya. Sisemi kwa ubaya, ila me naona kama Mona alikuwa na mchango mkubwa sana kwa Young Killer.”

Hayo ni baadhi tu kati ya mengi ambayo Stamina alifunguka kuhusu kufeli kimuziki kwa Young Killer.

0 comments:

Post a Comment