Pages

Subscribe:

Thursday, November 17, 2016

HUU NDIYO UFAFANUZI WA VIDEO YA CHIZI YA CHIN BEES


Kama wewe ni shabiki wa muziki mzuri na video kali za Bongo basi video ya “Zuzu” ni moja  ya video ambazo zinafanya vizuri kwa sasa na kupata airtime hadi katika luninga ya TRACE.

Sasa Kama kawaida katika kila video nzuri lazima kuwepo na mambo mengi ambayo yanaweza kujitokeza, na kwa upande wa ZUZU, Chin Bess akaona kwani...
shilingi ngapi akituambia tusiyoyajua kuhusu video ya Zuzu.

Akiongea na mwandishi, Chin Bees alifunguka na kusema kwamba Idea ya video ya “Zuzu” ilitolewa na director Gq baada ya kutumiwa ngoma na kusikiliza akatokea kuikubali ZUZU.

“Ile video ya zuzu idea alifanya Gq mwenyewe, mimi nilimtumia nyimbo akaniambia kwamba hii ngoma mi nimeipenda sana, akaniambia hapa lazima tufanye kitu, kwahiyo mpaka yunamtoa Gihcue Morogoro hadi Arusha ile idea alikuwa bado hajatupa, alivyofika ndio akatuambia kwamba inabidi niwe kama natoka demu dinner, alafu demu anakutana na muziki ambao hajaupenda, manzi anaanza kulalamika Baby mbona unanileta katika mazingira haya, ndipo hapo mimi inabidi nitoke niende kwenye bendi kumuimbia mtoto mzuri” Alisema Chin Bees

Mtangazaji ikataka kufahamu zaidi kwanini Chin Bees alitaka kazi yake ifanywe na Director Gq na sio kwa madirector wakubwa kama GodFather na wengine kibao, kwa upande wa Chin Bess akatujibu haya.

“Mi niliona kazi ya Gihcue kwenye Burger movie selfie kabla hata ya kutoka mimi nilikuwa exited na nikasema kwamba hii video lazima itafika mbali na ikafanikiwa, kwahiyo Gq ni mtu ambaye namkubali kwa uwezo wake wa kufanya kazi na nilikuwa nikiwish kufanya naye kazi, kunavideo moja ilibidi tufanye nae lakini haikufanikiwa sema this time nikafanikiwa, Meneja wangu Dwale aliongea na Gq na tukapatana nae vizuri hadi sasa navyokwambia video imekubalika Trace na wametoa Comments nyingi kuhusu uzuri wa video ya Zuzu” Aliongeza Chin Bees.

Mwisho kabisa Chin Bees alisema kwamba video ya “Zuzu” imegharimu pesa nyingi, japo hakutaja pesa yenyewe, kugharimu pesa nyingi katika Zuzu imetokana na Camera ambayo alikuwa anataka kutumia Gq Arusha haikupatikana ikabidi waagize kutoka Dar.

0 comments:

Post a Comment