Tuesday, December 13, 2016
SHAA ATOA SABABU YA MUZIKI WA SASA KUTODUMU TOFAUTI NA ZAMANI
Muziki wa Bongo Flava unaotoka sasa unaweza kuonekana kuwashika mashabiki ndani ya muda mfupi na video zake kuwa na mamilioni ya views kwenye Youtube, lakini hakuna anayeweza kubisha kuwa haudumu kama zamani? Kwanini?
Shaa anauita muziki wa leo ‘bubblegum’ na kwamba huwezi kuufananisha na ule uliotoka miaka mitano au saba tu nyuma. “Ni kazi ambazo hata miaka 20 kuanzia sasa bado unaweza ukazicheza na ukawa...
on point,” Shaa alikiambia kipindi cha The Playlist cha Times FM kuhusu nguvu ya muziki wa zamani.
“Nakumbuka wikiendi iliyopita nilikuwa kwenye event fulani wakawa wanagonga old school, wakagonga Mkasi, yaani the place went crazy. Mimi naona kama vile sound wise, muziki, quality inashuka kwenye baadhi ya wasanii. Kitu ambacho naona tumeendelea sasa hivi muziki umekuwa biashara especially kwenye upande wa msanii, endorsement deals nikimaanisha, unaweza ukajiuza online, Youtube, unaweza kuuza views,” aliongeza.
Labels:
HABARI & UDAKU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment