Msanii
mkongwe wa muziki Ray C ameamua kuyapotezea yale yanayozungumzwa katika
mitandao ya kijamii baada ya jana mtandao wa Global Publisher kuandika
taarifa inayodai kuwa muimbaji huyo wa wimbo ‘Milele’ anajiuza.
Kwa
mujibu wa taarifa za mtandao huo zinadai kuwa haikuwa kazi rahisi
fuatilia mkasa huo mpaka walipowatumia Kamanda wa Oparesheni Fichua
Maovu (OFM) ya...
mtandao huo.
Muimbaji huyo ambaye ameweza
kupambana kuachana na matumizi ya Madawa ya kulevya, ameona siyo vyema
kukaa kimya na kuamua kuzungumza kuhusu issue inayozungumzwa.
Kupitia mtandao wa Instagram, Ray C ameandika:
Maisha
ni Safari ndefu,unapoona hali ya maisha inakuwa ngumu basi ujue kuna
utimilifu na ukamilifu mbele yako, usikatishwe tamaa na maneno ya
binadamu wenzio ambao wana miguu miwili kama wewe na wameumbwa na
yuleyule aliekuumba wewe na ambao nao hawajui hatma ya maisha yao kama
vilevile usivyojua hatma yako,kesho yako usivyoijua basi ujue hakuna
binadamu anaeifahamu kesho yake itakuwaje!
kumbuka mtabiri na mwongozaji
wa maisha yako ni mmoja tu aliekuumba wewe na ndie peke yake wa
kumtegemea katika kila jambo maishani mwako,dunia na watu wake na vitu
vyake na mambo yake yataendelea kuwepo tu muhimu ni wewe kujua unasimama
upande upi salama katika kufanikisha kile unachokidhamiria kwenye
maisha yako, muhimu ni kuwa na imani matumaini na ujasiri wa kufanikisha
jambo lako,funga skio la nafsi haribifu za utabiri wa dunia za
munguwatu na sikiliza nafsi yako ndani yako iliyo ya ukweli na nia
kufikisha malengo yako maishani mwako, jiamini jikubali sema kwa nguvu
ya Mungu ntafanikisha nitakalo maishani!
ongea na Mungu wako katika kila
jambo mshirikishe yeye Kwani kuna nguvu ya Mungu inayotembea na sisi
wakati wote ni kuamini tu kwamba mbele yake yeye muumba mwenye dunia
yake hakuna linaloshindikana chini ya jua!kuwa na imani na yeye
tu!hakuna mwingine mwenye upendo wa kweli kama Mungu.
Muimbaji huyo kwa sasa amekuwa akijichimbia katika studio za Wanene kuandaa kazi zake mpya ambazo bado hajazizungumzia.
Tuesday, December 20, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment