Friday, December 9, 2016
MAMLAKA YA HIFADHI NGORONGORO YAJITETEA KUHUSU UPOTEVU WA FARU JOHN
Uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro mkoani Arusha umesema umeanza kutekeleza agizo la Waziri Mkuu la kutaka kuwasilisha nyaraka zote za kumhamisha Faru ajulikanae kama John na maelezo ya kupotea kwake.Akizungumza na TBC, Mhifahi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Dkt Fedrick Manonge amesema japo amepewa muda mfupi sana wa kuwasilisha taarifa hizo lakini wanajitahidi kuzikamilisha.
“Kwahiyo yeye alimuagiza waziri wa maliasili ni anataka nyaraka husika na anataka maelezo ya kilichotokea. Kwahiyo kwasababu inakuwa ngumu sana kusema details zingine kwasababu...
ilisemwa na nyie mlisikia hakukuwa na information za kumridhisha mheshimiwa waziri mkuu ndiyo maana akatoa hayo maelekezo.
Kwahiyo mi nadhani kimsingi nikusubiri matokeo ya huo uchunguzi ambao kwa kweli ametoa siku chache sana, serikali ya awamu ya tano haina vificho eeh itaonekana wazi kilichotokea,” alisema Manonge.
Labels:
HABARI & UDAKU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment